Katika siku ya kuadhimisha Changia Damu Salama, wanafunzi wa shule na madrasa mbalimbali wamejitokeza kwa wingi katika Hospitali ya Bombo kutoa damu na kusaidia kuokoa maisha. Wanafunzi hawa wameonyesha moyo wa uzalendo na huruma kwa jamii kwa kujitolea damu itakayosaidia wagonjwa wenye mahitaji maalum, akiwemo mama wajawazito, watoto wachanga, na waathirika wa ajali.

"Tunawapongeza vijana hawa kwa kushiriki katika tukio hili muhimu na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii. Kwa pamoja, tunaweza kuokoa maisha na kuleta matumaini kwa wenye uhitaji."

Shirika la Afya linawataka watu wote kuendelea kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara. Changia damu leo, toa zawadi ya maisha!