Wanachama wa Taasisi ya Jai wamepongezwa kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika siku ya Changia Damu Salama iliyofanyika katika Hospitali ya Bombo. Ushiriki wao umeleta faraja na tumaini kwa wagonjwa wenye uhitaji, na kuwa mfano wa kuigwa katika kujenga jamii yenye kujali.

"Taasisi ya Jai inaendelea kuonyesha dhamira ya dhati kwa kuwahamasisha wanachama wake kushiriki katika shughuli za kijamii, na siku hii ya damu ni ushahidi wa moyo wa kujitolea kwa maslahi ya wengi."

Shukrani kwa wanachama wa Jai kwa kuwa sehemu ya mabadiliko. Kila tone la damu linasaidia kuokoa maisha