Tarehe 17 Februari 2025, Mkoani Tanga, katika viwanja vya Urithi Tanga Museum, kulifanyika sherehe maalum za kuadhimisha siku ya mwanamke, sambamba na ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan. Katika sherehe hizi, Jamiiatul Akhlaaqul Islaam (JAI) ilifanya jambo la kipekee ambalo lilivutia na kukubalika na washiriki wote wa kongamano hilo.

Katika mkutano huu, JAI ilikua sehemu ya juhudi kubwa za kijamii kwa kuendesha zoezi la uchangiaji damu kwa wadau na washiriki wa kongamano. Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kuongeza idadi ya damu katika benki ya damu salama ya Tanga, ili kuokoa maisha ya wananchi. Huu ulikuwa ni mchango mkubwa kwa jamii, ambapo JAI ilifanikiwa kuchangia na kuongeza damu muhimu kwa hospitali na vituo vya afya.

Zoezi hili liliratibiwa na Naibu Amiri wa JAI pamoja na kamati nzima ya JAI Mkoa wa Tanga, na lilikua na mafanikio makubwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Wadau waliguswa na juhudi hizi za JAI, na wengi walijitokeza kutoa pongezi kwa taasisi hiyo. “Tunaipongeza taasisi ya JAI kwa kujitoa kwake na kwa kipaumbele cha kuchangia na kuokoa maisha jamii nzima,” alisema mmoja wa washiriki.

Shughuli hii ilionesha wazi kwamba Jamiiatul Akhlaaqul Islaam (JAI) inatambua umuhimu wa kujitolea na kuchangia katika shughuli za kijamii ambazo zinahusiana na afya na ustawi wa jamii. Kwa hivyo, JAI ilionyesha kwa vitendo jinsi taasisi za kijamii zinavyoweza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya afya ya wananchi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Kwa mafanikio haya, JAI inatoa wito kwa taasisi na watu binafsi kuendelea kuchangia na kushirikiana kwa pamoja ili kuokoa maisha na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Zozi hili la uchangiaji damu ni mfano wa ufanisi wa juhudi zinazofanywa na JAI katika kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma za afya bora na kuokoa maisha ya wanyonge.